Saturday, 6 June 2015

FAIDA ZA ASALI


Asali kama chakula na pia dawa ni dhana  kongwe katika historia ya mwanadamu. Kwa mfano yapata miaka 4,000 (elfu nne) iliyopita madakatari wa tiba wa Kimisri na wale wa Sumarani waliitumia asali kutibu magonjwa mbali mbali kama vile vidonda vya tumnbo na vile vya kawaida, magonjwa ya macho, ngozi na yale ya tumbo.

 Historia pia imerikodi matumizi kama hayo kwa watu wa Uchina, Ugiriki, Roma, n.k. Hippocrates, baba wa tiba kwa nchi za magharibi pia alitumia asali kutibu
magonjwa mbali mbali, vile vile Ibn Sina, mfalme wa tiba kutoka katika ulimwengu wa nchi za Kiislamu ameorodhesha faida nyingi za matumizi ya asali, katika buku lake la tiba
maarufu "The Canon of Medicine".

 Miongoni mwa faida alizotaja Ibn Sina katika buku hilo
(Misingi ya tiba) ni kuweka mwili katika hali ya ujana, kuongeza uwezo wa kukumbuka
mambo, kuleta furaha, kusaidia usagaji wa chakula kuongeza hamu ya kula chakula, na
kuongeza uwezo wa mtu kuzungumza vizuri. Elimu ya Sayansi (ya kisasa) nayo
imemwezesha mwanadamu kufahamu kwa kina ubora wa asali. Kwa mfano, tangu
mwaka 1937 wanasayansi walijua kwamba wingi wa sukari iliyomo katika asali
(76gllooml), tindikali (acidity, Ph = 3.6-4.2), na kuwemo kwa baadhi ya kemikali
zinazotokana na viumbe hai (Organic Compounds).

 Ni sababu zinazoifanya asali kuwa ni dawa. Yaani inaweza kuulinda mwili usipate maradhi na pia inaweza kuviua vijidudu vya maradhi vilivyomo ndani ya mwili wa mgonjwa.
Zaidi ya hayo, sayansi inatujulisha kuwa, asali inamchanganyiko wa virutubisho na
kemikali za aina mbali mbali. Baadhi ya vitu hivyo ni sukari, vitamini, amino acids (vitu
vinavyotengeneza protini), vimeng'enyo (enzymes), homeni (hormones).

Follow us on FaceBook